Rapa Rich Homie afariki dunia

Rapa Rich Homie afariki dunia

Rapa Rich Homie Quan (34) amefariki dunia leo Alhamisi Septemba 5, 2024 na taarifa za kifo cha msanii huyo zilianza kusambaa mtandaoni, huku wasanii wenzake kama Boosie Badazz na wengine wakituma salamu za pole katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tovuti ya TMZ, Quan amefariki akiwa nyumbani kwake Atlanta, huku familia yake wakithibitisha.

Jacquees, ambaye alishirikiana na mkali huyo kwenye wimbo kama ’Rich As In Spirit’, “Come Thru” na “Feel It,” aliandika kupitia mtandao wa X , “Pumzika kwa amani, kaka yangu, Rich Homie Quan. Nakupenda maisha yote.”

Taarifa za awali zinasema kuwa kifo cha rapa huyo Quan zimesababishwa na kutumia dawa za kulevya ambazo zimesababisha moyo kushindwa kufanya.

Quan alipata umaarufu kupitia "Type of Way" ya mwaka 2013. Wimbo huo uliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati ya Billboard Hot 100, huku video zake zikikusanya zaidi ya watu 308 milioni waliotazama kwenye YouTube. Mwaka uliofuata, yeye na Young Thug waliona mafanikio makubwa na wimbo wa "Life Style" ambao walishirikishwa na kundi la Rich Gang lililopo chini ya Mkongwe Bird Man ambapo wawili hao walileta mafanikio mengi ndani ya lebo hiyo kabla ya kutengana mnamo 2015.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags