Rapa 6ix9ine arudishwa jela

Rapa 6ix9ine arudishwa jela

 

Rapa Daniel Hernandez maarufu 6ix9ine amerudishwa jela kwa siku 30 baada ya kukiuka masharti ya kifungo cha nje alichopewa na Mahakama mwaka 2019.

Mahakama imechukua hatua hiyo baada ya 6ix9ine kusafiri kwenda Las vegas bila ruhusa, nakushindwa kuhudhuria vipimo vya dawa za kulevya huku akikutwa akiendelea na matumizi ya dawa hizo.

Kwa sasa rapa amefungwa katika gereza la Metropolitan Detention Center “MDC” lililopo maeneo ya Brooklyn, New York ambapo amempangiwa kufika Mahakamani Jumanne ya Novemba 12 mwaka huu.

6ix9ine aliachiwa huru mwaka 2019 na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha nje baada ya kukiiri na kukubali kutoa ushirikiano kwa Mahakama.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags