Ramadhani Brothers washindwa kutwaa ubingwa Australia’s got talent

Ramadhani Brothers washindwa kutwaa ubingwa Australia’s got talent

Watanzania Ibrahim na Fadi Ramadhani maarufu kama Ramadhani Brothers, ambao ni washindi wa 'Golden Buzzer' kwenye mashindano ya vipaji ya Australia's Got Talent 2022 (AGT), wameshindwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo katika fainali zilizoruka usiku wa kuamkia leo.

Ramadhani Brothers wanaweza kuwa sio washindi, lakini wameshinda mioyo ya wapenzi wengi wa mashindano hayo, hususan wana-Afrika Mashariki.

Katika hatua nyingine, washindi wa mashindano ya AGT wametajwa kuwa ni kundi la mabinti 19,  wanaojiita Acromazing walioshinda mbele ya wakali wengine Oleg, mchekeshaji Emo Majok, Walison Muh, staa chipukizi wa muziki Sienna Katelyn pamoja na Ramadhani Brothers

All in all wamejitahidi mno kwa hatua waliofikia wanahitaji pongezi kubwa sana kwao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags