Rais wa ‘soka’ aliyembusu mchezaji wa kike ajiuzulu

Rais wa ‘soka’ aliyembusu mchezaji wa kike ajiuzulu

Hatimaye Rais wa Shirikisho la Soka Hispania, Luis Rubiales amejiuzulu kufuatia sakata la kumpiga busu mdomoni mchezaji wa Timu ya Taifa ya wanawake Jenni Hermoso, kitendo ambacho kilizua taharuki.

Rubiales amechukua uamuzi huo baada ya kuandamwa kwa week tatu na kashfa za kumpiga busu mdomoni mchezaji huyo wakati ‘timu’ ya taifa ya Uhispania walipoibuka washindi wa Kombe la Dunia la Wanawake.

Aidha Rais huyo alikosolewa vikali kwa kitendo hicho na kutakiwa kujiuzulu na mashabiki mbalimbali wa soka la Hispania, hatua ambayo mwanzoni inadaiwa kuwa alikataa kujiuzulu lakini sasa abwaga manyanga.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags