Rais Biden Aambukizwa Virusi vya Corona

Rais Biden Aambukizwa Virusi vya Corona

Rais wa Marekani Joe Biden ameripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19 hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani.

Rais Biden alikuwa tayari ameshatumia dozi mbili za kujikinga na Covid- 19 aina ya Pfizer muda mchache kabla ya kuingia madarakani ambapo chanjo ya kwanza alichanja mwezi Septemba 2021 na ya pili alichanja mwezi Machi mwaka huu.

“Rais Biden amekutwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 na amechanjwa vizuri ingawa amekumbwa na dalili za maambukizi ya virusi hivyo.” Alisema Msemaji wa Ikulu Karine Jean –Pierre.

Aprili 30, 2022 Rais Biden alihudhuria shughuli yenye mkusanyiko wa watu wengi katika Ikulu ya White House akiwa hana tahadhari yoyote ya kujikinga na maambukizi ya Uviko -19 na kusema kuwa anatambua hatari ya virusi hivyo lakini lilikuwa ni jambo la thamani kwa yeye kushiriki katika tukio hilo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags