Taarifa kutoka Misri ambapo taasisi ya Kitaifa ya Lishe nchini humo imetoa wito kwa watu kula miguu ya kuku badala ya nyama.
Uamuzi huo umekuja kutokana na gharama ya miguu ya kuku kuwa nafuu zaidi, hatua iliyowakasirisha wananchi wengi wakidai ni alama ya umasikini uliokithiri nchi humo.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti, nchi hiyo ya Afrika Kaskazini inakabiliwa na mfumuko wa bei mbaya zaidi katika kipindi cha miaka mitano, hivyo kusababisha Wamisri wengi kushindwa kumudu kuku ambacho ni chakula kikuu.
Leave a Reply