Radi yaua wachezaji, Kenya

Radi yaua wachezaji, Kenya

Wachezaji wawili wa soka wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi walipokuwa wakicheza mechi katika kaunti ya Kisii magharibi mwa Kenya, vyombo vya habari nchini  humo vimeripoti

Huku wachezaji wengine wawili walipelekwa hospitali kwa matibabu ya dharura baada ya kupata majeraha wakati wa mashindano hayo.

Afisa mmoja wa shirikisho la soka nchini alinukuliwa akisema kuwa timu hizo zilikuwa na mechi ya kirafiki mvua ilipoanza kunyesha

"Inasikitisha sana kwamba walipoteza maisha wakati wakicheza mchezo ambao waliupenda zaidi. Kama maafisa wa shirikisho, tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia zilizoathiriwa,” gazeti la Daily Nation lilimnukuu mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Kenya Evans Akang’a akisema.

Aidha afisa huyo alizitaka mamlaka hizo kufunga vifaa vya kukamata radi katika maeneo ya umma ikiwemo shule zinazofanyika mechi ili kupunguza matukio hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags