R.Kelly ahamishwa gereza

R.Kelly ahamishwa gereza

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani R.Kelly ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyanyasaji wa kingono, wiki iliyopita amehamishwa gereza kutoka Chicago correctional center hadi North Carolina nchini humo.

Kwa mujibu wa Hollywood Unloacked, "benjamin o'cone" ambaye ni msemaji wa gereza la NC ambapo  kelly anatumikia kifungo kwa sasa alitoa taarifa siku ya jumatatu kuwa.

“R.kelly alihamishiwa katika gereza la butner fci (N.C) ambako kuna ulinzi mdogo lakini atapatiwa huduma bora na muhimu za kibinadamu pamoja na matibabu kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata akiwa gereza la chicago. hivyo tunaamini Butner fci watamjali na kulifanyia kazi hilo”

Ikumbukwe tuu mwaka 2022 R.kelly alihukumiwa jela miaka 30+1 kwa unyanyasaji wa kingono lakini pia feb mwaka huu amehukumiwa miaka 20 jela kwa kesi iliyoitwa ulaghai wa kingono, hivyo atatumikia miaka yote kwa pamoja






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags