Primeboy akamatwa tena, kisa kifo cha Mohbad

Primeboy akamatwa tena, kisa kifo cha Mohbad

Rafiki wa karibu wa marehemu mwanamuziki Mohbad kutoka nchini Nigeria, Primeboy, amekamatwa tena na polisi baada ya kutajwa kuhusiaka katika kifo cha Mohbad.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini Nigeria vimeripoti kuwa Primeboy alikamatwa siku ya jana Jumanne Machi, 12 alipokwenda katika idara ya upelelezi wa jinai ambapo huenda kila wiki kwa ajili ya kusaini.

Mohbad (27) alifariki Septemba 12 katika mazungira ya kutatanisha tukio ambalo lilizua mtafaruku nchini humo, na kupelekea baadhi ya mastaa kukamatwa kutokana na kuhusishwa na kifo hicho, akiwemo promota Sam Larry pamoja na Naira Marley. Ambao kwa sasa wapo uraiani baada ya kuachiwa kwa dhamana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags