Popo wa New Zealand ashinda tuzo

Popo wa New Zealand ashinda tuzo

Popo mmoja ametajwa kuwa ndiye ndege wa mwaka wa New Zealand, katika hali ya kutatanisha ambayo imesababisha lalama kali mitandaoni nchini humo.

Popo mwenye mkia mrefu alikuwa amejitosa na kutwaa taji hilo kufuatia kura ya mtandaoni.

Waandalizi wa shindano hilo walikuwa wamejumuisha popo, mmoja wa mamalia wachache wa asili wanaoishi nchi kavu, ili kuinua hadhi yake kama spishi iliyo hatarini kutoweka.

Wapenzi wa ndege waliokasirika walilalamika kwenye Twitter, wakiita ushindi huo kama “mchezo “, “uchaguzi ulioibiwa”, pamoja na maneno mengine yasiyoweza kuchapishwa.

Wengine kwenye mitandao ya kijamii pia waliona kuwa ni ushindi unaohitajika sana wa mahusiano ya umma kwa popo, baada miaka miwili yenye changamoto.

Lakini kikundi cha mazingira cha Forest and Bird, ambacho huandaa shindano hilo kila mwaka, kilisema kujumuishwa kwa popo sio dhamira ya kurejesha hadhi ama sifa za mnyama huyo kutokana na janga la corona

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags