Polisi wamrudisha Niffer Dar baada ya kujisalimisha

Polisi wamrudisha Niffer Dar baada ya kujisalimisha

Jeshi la Polisi limemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam mfanyabiashara wa mtandaoni, Jenifer Jovin maarufu Niffer baada ya kujisalimisha polisi jana.

Mfanyabiashara huyo alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza Jeshi hilo kumhoji kwa kosa la kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam bila kibali.

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16, majeruhi 86 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2024 jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Anania Amo amesema Niffer amekamatwa na polisi baada ya kujisalimisha jana.

“Alijisalimisha jana baada ya kumtafuta, tayari tumemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam,”amesema.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

(Imeandikwa na Sharon Sauwa)






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags