Polisi wakanusha kumshikilia Eric Omondi

Polisi wakanusha kumshikilia Eric Omondi

Baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikimuonesha mchekeshaji wa Kenya, Eric Omondi akiwa amedakwa na polisi, mpenzi wa mchekeshaji huyo, Lynne Njihia amedai kuwa polisi wamekataa kuwa hawajamkamata Omondi.

Kupitia insta story ya mwanadada huyo ameweka wazi kuwa amefika kituo cha Polisi cha Kati alichodaiwa kupelekwa Omondi baada ya kukamatwa lakini polisi wa kituo hicho wamekata kuhusika na tukio hilo.“Ni bahati mbaya sana mpenzi wangu Eric alikamatwa mapema leo na mpaka sasa hatuwezi kumtafuta kabisa tupo kituo cha Polisi cha Kati alikoletwa na ushahidi wote upo mtandaoni lakini polisi wanaendelea kutuchezea, swali letu wamempeleka wapi? Eric Omondi na kwanini wanamficha,” amehoji mwanadada huyo.

Video iliyosambaa mtandaoni mapema leo ilionyesha Polisi wakiwa wamemshikilia mchekeshaji huyo kwa nguvu, wakati alipokuwa kwenye maandamano yanayoendelea nchini humo ya kupinga ongezeko la kodi katika Muswada wa Fedha wa 2024/ 2025.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post