Pogba na mkewe wapata mtoto

Pogba na mkewe wapata mtoto

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba amewapiga mashabiki zake na kitu kizito baada ya kutumia ukurasa wake wa Instagram kutujuza taarifa njema za kumpata mtoto wa tatu, akisema kuwa “ana furaha sana kuwa baba wa watatu”.

Mwamba huyo ali-share picha mbalimbali akiongea na mkewe kupitia Facetime wakati akielekea hospitali huku akiambatanisha na maneno yaliyo someka “Al Hamdullilah mwanakaya mpya wa Familia ya Pogba amewasili, najivunia sana malkia wangu nimefurahi sana Baba watatu” ameandika Pogba



Ujio wa binti yake unamfanya Pogba kuwa na watoto watatu wakiwemo Labile aliezaliwa mwaka 2019 ikiwa ni mwaka ambao kiungo huyo wa Juventus alifunga ndoa, pamoja na Keyaan aliyezaliwa mwaka 2020.

Hivi sasa kiungo huyo anasumbuliwa na majeraha yaliyo sababisha mwanzo mgumu kwa kiungo huyo wa Juventus ya nchini Italia aliyojiunga nayo baada ya kuachana na miamba ya England klabu ya Manchester United.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags