Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele sanaa ndiyo kazi ambayo inawatoa watu wengi hususani vijana kulingana na juhudi ambazo wanazifanya.
Tambua kuwa unapozungumzia Sanaa always hua inasimama kwenye masuala ya Ubunifu, Uvumbuzi, nk ili uweze kufanya vizuri zaidi kwenye sector hii basi amini kwamba Creativity imeshika nafasi kubwa sana.
Its Monday na leo kwenye makala ya Kazi, ujuzi, maarifa na kukutanisha na Binti anayefahamika kwa majina Placidia Akyoo anayejishughulisha na kazi za sanaa akiwa amebase kwenye masuala ya Typography Arts.
Placidia Akyoo ni binti aliyemaliza Chuo cha IFM hivi karibuni alipokuwa akichukua course ya Bachelor Of Insurance and Risk Management chuoni hapo.
Licha ya kusomea course hiyo lakini Placidia anajihusisha na kazi za sanaa ikiwemo ya uchapaji (Typography), lakini pia anauwezo wa kudesign office pamoja na mapambo ya nyumbani yaani (home decoration).
Typography Arts hii ni kazi inayohusisha zaidi sanaa ya Maneno na matukio mbalimbali ikiwemo ya faraja au maneno yenye Hamasa yaani (Inspiration )nk.
Akizungumza na Jarida la Mwananchi Scoop, Placidia amefunguka mambo mbalimbali yanayohusiana na kazi hiyo ambayo anaifanya ikiwemo passionate ndiyo imepekea yeye kuanza kufanya shughuli hiyo.
Vile vile alisema ni kitu ambacho anacho kwani yeye anapenda sana kuandika andika hususani kucreate maneno tofauti tofauti hivyo ni ubunifu ambao ameunza muda mrefu kutokana nayeye kuipenda kazi hiyo.
Aidha amezungumzia hali ya soko ya kazi hiyo na amebainisha kuwa bado soko liko chini mnoo, kwani kwa mwezi anaweza kuuza picha mbili au tatu jambo ambalo haliridhishi.
Vilevile alisema licha ya kua na hali mbaya kisoko lakini kwa upande wake anaamini atatoboa tu kadri siku zinavyozidi kwenda akizidisha ufanisi wa kazi yake anaimani atafika mbali zaidi.
Hata hivyo alizungumzia changamoto za kazi hiyo alisema watu wengi bado hawajaifahamu sanaa hiyo jambo ambalo linaleta ugumu katika kupata wateja.
“Changamoto kubwa bado soko halijatambulika vizuri watu wengi hawana elimu ya kutosha juu ya kazi hii hivyo ni changamoto hata katika masuala ya kupata wateja”alisema.
Aidha alianisha malengo yake kuhusiana na kazi hiyo mojawapo ni kuhakikisha siku moja anakuja kuwa mfanyabiashara mkubwa na maarufu hapa nchini.
Sambamba na hayo alisema mapambano ni makubwa sana ambayo anayapitia licha ya kufanikiwa kuchukua Tuzo kwenye mashindano ya IFMAS yaliyoandaliwa na Institute of Financial Management Arts society ambayo yalihusisha vipaji vya wanafunzi walioko Chuoni kwao.
Katika mashindano hayo aligombania Tuzo ya Best Writer kutokana na yeye alikua akijihusisha na masuala ya maandishi na kufanikiwa kunyakua Tuzo hiyo.
“Mapambano ni makubwa mnoo nimekutana disappointment nyingi, discarrage nyingi sana lakini nilipambana hadi kufika hapa na sio kitu kidogo nimeshakatishwa tamaa sana lakini nilisimama alone na nikafanikiwa”alisema.
Vile vile alizungumzia jinsi familia yake inavyomsapoti kwenye kazi anayoifanya na kubainisha kuwa familia yake inamsaidia kwa kiasi chake kwani mara nyingi anapokwama hua wanajitoa kumsaidia.
Hata hivyo alisema badoo jamii haina uelewa mpana dhidi ya kazi anayoifanya kwani ndiyo jambo ambalo linachangia kuwepo kwa ugumu wa kazi hiyo.
Je wew ni binti mwenye vipawa gani?
“Mimi ni msichana ambaye najiamini, najitoa sana, ninauwezo wa kufanya kazi zangu bila kusimamiwa, lakini pia najituma hasa na napangilia sana mambo yangu kweani hua nakwenda kwa target ambazo huwa najiwekea”alisema.
Placidia ni binti ambaye anavipaumbele vyake pia kwenye maisha yake ikiwemo kuja kuwa Mwanamke bora katika familia yake hapo baadaye.
Ndoto zake
Placidia ni binti mwenye ndoto za kujakuwa mfanyabiashara mkubwa wa kike hapa nchini akiwa na nia ya kuwasaidia vijana wengine wenye vipaji wanaochipukia.
Ebwana eeh!! Kupitia makala ya wiki hii kuna mafunzo makubwa utakua umeyapata nikukumbushe tu ili ufike mbali zaidi hakikisha unajibidiisha katika kufanya kazi na kusimamia misimamo yako hakika utatoboa.
Have a nice Monday!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Gloria
Hongera rafiki Yng,daima ufike mbali na ufanikiwe
Monica
Good work placia I really appreciate your work🥰🥰
Franciscasarah francis
I really appreciate your movements and u real motivate me so much 💕💖
Esther
Congratulation my dear you can make it
Esther
Congratulation my dear you can make it