Peter Okoye avunja ukimya, awataka mashabiki kuwa na subira

Peter Okoye avunja ukimya, awataka mashabiki kuwa na subira

Baada ya mwanamuziki kutoka Nigeria, Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ kuweka wazi kuwa kundi la P-Square limesambaratika kwa mara nyingine, kwa upande wa Peter Okoye, ‘Mr P’ amevunja ukimya huku akiwataka mashabiki wake kuwa na Subira kuhusiana na suala hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr P amechapisha ujumbe ukieleza kuwataka mashabiki wawe na subira kufuatia na gumzo la kusambaratika kwa kundi hilo, huku akidokeza ujuo wa album ambayo itajibu maswali yote.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kuwa kundi la #PSquare limegawanyika kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.

Kundi P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka jana kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamegawanyika tena.

Wawili hao walitamba na ngoma zao kama ‘Taste The Money (Testimony )’, ‘Personally’, ‘Forever’ pia wamewahi kutoa kolabo na mwanamuziki #Diamond wimbo uitwao ‘Kidogo’






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags