Pete alia na ndoa za waigizaji Nigeria kuvunjika

Pete alia na ndoa za waigizaji Nigeria kuvunjika

Muigizaji mkongwe kutoka nchini Nigeria Pete Edochie ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 76, ameonesha kusikitishwa na ongezeko la kuvunjika kwa ndoa za baadhi ya waigizaji movie kutoka Nigeria.

Pete ameeleza hisia zake hizo za  kusikitika wakatia  akizunguma kwenye ‘podikasti’ ya ‘WithChude’, akidai kuwa kwenye Tasnia ya Filamu nchini Nigeria wasichana wengi walioolewa miaka miwili au mitatu iliyopita wamewaacha waume zao.

Katika kusema hayo Pete akatolea mifano ya baadhi ya ndoa zilizo mshagaza  baada ya kusikia zimevunjika, zikiwemo ndoa za waigizaji kama vile Chioma Akpotha, Ireti Doyle na Tonto Dikeh.

Pete amedai kuwa  wanawake wanatakiwa kuchukulia swala la harusi na ndoa kwa uzito, kuvumiliana kwenye, mabaya na mazuri.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags