Peru yatangaza siku 30 za hali ya hatari

Peru yatangaza siku 30 za hali ya hatari

Serikali ya Peru imetangaza siku 30 za hali ya hatari nchi nzima. Katika tangazo hilo la jana, Waziri wa Ulinzi Alberto Otarola alisema haki ya kukusanyika, kutoingiliwa majumbani na uhuru wa kutembea vimesitishwa.

Pia kumewekwa marufuku ya kutotoka nje usiku. Hatua hiyo inakuja wakati maandamano yakiendelea kwa siku kadhaa sasa tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Pedro Castillo na kutiwa nguvuni tarehe 7 Disemba.

Castillo bado yuko jela kungojea mashitaka ya ufisadi na njama za uasi dhidi yake. Aliyekuwa makamu wake, Dina Boluarte, aliapishwa kuwa rais wa sita wa Peru baada ya Castillo kufungwa jela.

 Boluarte amejaribu kuwashawishi waandamanaji kwa kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi, lakini hadi sasa hali haijatulia. Wafuasi wa Castillo na wapinzani wao wanataka uchaguzi wa haraka badala ya kumtambuwa Boluarte kama rais wao.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post