Mwanamuziki wa Afrika Kusini, Khulekani Nxumalo 'Pcee' anayetamba na ngoma ya 'Kilimanjaro', amesema wakati anatoa wimbo huo hakuwa anamaanisha mlima uliopo Tanzania badala yake alimaanisha mwanamke anayejiremba.
Hayo ameyasema wakati akifanya mahojiano na redio NRG iliyopo Kampala.
"Nikiwa nazungumzia Kilimanjaro, sikumaanisha mlima Kilimanjaro, kuna lugha moja huko Afrika Kusini. Kwa hiyo unaposema, msichana huyu, anajiremba kwa kuosha uso wake na maziwa au labda anatumia vipodozi safi,"
Anasema msichana anapokuwa akitumia vipodozi mara kwa mara kwa lugha ya kuzulu ndivyo hutamkwa na kusikika kama Kilimanjaro.
Baada ya wimbo huo kupendwa na kufanya vizuri Tanzania anasema ilimshangaza ndipo baadaye akafahamishwa kuwa watu amdhani anauimba mlima.
"Watu walivutiwa sana wakaamka tu na kuanza kukimbia na hiyo Kilimanjaro, walipoangalia namba za Tanzania nilishituka sana, niliambiwa kaka bado upo namba moja Tanzania. Ni miezi miwili nilikuwa namba moja,"amesema
Hata hivyo anasema alipoanza kupokea mialiko Tanzania alishangaa kuona watu wakishangilia na kuupenda wimbo ndipo akaambiwa Kilimanjaro ni jina la mlima hivyo linamaana .
Utakumbuka wimbo huo uliachiwa mwaka mmoja uliopita na hadi sasa kwenye mtandao wa YouTube umetazamwa mara milioni 4.1
Leave a Reply