Patrick Aussems kocha mpya Singida BS

Patrick Aussems kocha mpya Singida BS

Aliyewahi kuwa ‘kocha’ mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems maarufu pia kama Uchebe, raia wa Ubelgiji amerejea nchini, safari hii akiwa na Singida Black Stars inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uongozi wa ‘klabu’ hiyo zamani ikijulikana kama Ihefu FC umethibitisha kuingia makubaliano na kocha Aussems ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi kuanzia msimu mpya wa 2024/25 kwa kandarasi ya awali ya msimu mmoja hadi Juni 30, 2025.

Aussems ana leseni ya UEFA PRO na uzoefu wa kufundisha klabu kubwa barani Africa, Ulaya na Asia, zikiwemo timu za Al Hilal Omdurman (Sudan), Simba SC (Tanzania), AFC Leaopards (Kenya), Shenzhen Ruby (China), ETG (Evian Thonon Gaillard) FC & Angers SCO FC ya Ufaransa.

Pia amefundisha timu za taifa zikiwemo za Nepal na Benin. Kocha Aussems amewahi pia kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Marbella FC ya Hispania.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post