Paschalia Anselimo (TUDARCo):  Biashara mitandaoni fursa mpya kwa vijana

Paschalia Anselimo (TUDARCo): Biashara mitandaoni fursa mpya kwa vijana

Kwa sasa barani Afrika na duniani kwa ujumla kuna ukuaji mkubwa wa biashara hasa za mitandaoni na inaonekana kuwa fursa kwa vijana wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNCTAD), DK Mukhisa Kituyi mwaka 2018 alieleza kuwa ukuaji huo barani Afrika ni asilimia 18 kwa mwaka lakini anahoji hali hii,“Huenda ni kweli kwamba watu milioni 21 wananunua huduma mtandaoni.

Pia alisema huenda ni kweli kuwa watu milioni 134 wanatembelea mtandao wa Facebook lakini kweli kabisa kuwa hakuna kiwango cha maana cha huduma zinazouzwa kutoka Afrika mtandaoni.

Hata hivyo kwa miaka ya hivi karibun sote tumeshuhudia jinsi ambavyo vijana wengi wameamka na kuanza kufanya biashara huko mitandaoni na imeonekana kuwalipa zaidi

Paschalia Anselimo (22) mwanafunzi aliyehitimu masomo yake ya Business Administration and Management in Marketing pale Chuo cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (TUDARCo).

Kwa sasa Paschalia ni mfanyabiashara wa matunda inayojulikana kwa jina la Fruitbox Tanzania.

Mwanadada huyu amekuwa akiifamya biashara hiyo kwa njia ya mitandao, najua hapa utajiuliza maana ulishazoea kuna biashara ya nguo na vyakula mara nyingi ndizo zikifanywa sana na watu huko mitandaoni.

 

Paschalia anauza matunda yaani fresh fruit kwa kuzingatia tunda gani lichanganywe na tunda gani ili kutatua nini katika mwili.

“Hii ni online business kwa sasa na tumejikita haswa kwenye events mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam, kwangu mimi hii ni fursa mpya ambayo vijana wanapaswa kuichangamkia,” anasema

Anasema kwa mara ya kwanza, alipata wazo la kuuza matunda akiwa A-level mwaka 2018, akiwa anaandaa mipango na mikakati baada ya kumaliza shule atafanya nini.

“Na jina la kwanza wakati naandaa mikakati ya "life after school" nilitaka kuiita Turuda Matunda. Lakini mambo yakaingiliana, hivyo sikuanzisha. Hadi mwaka 2020 mwishoni, nilikua na rafiki yangu kipenzi ambae pia ni business partner wangu, Janeth David, akanikumbusha.

“Ndipo nilipoamua kukaa chini nikadraft tena wazo, bajeti mpya ya kiuhalisia na nikaanza kuuza chuoni pale TUDARCo na nilipomaliza nikaona iwe tu mtandaoni mpaka pale tutakapopata physical place,” anasema

Changamoto

Anasema moja ya changamoto anayokumbana nayo ni watu kutokuwa na imani kaabisa na biashara za mitandaoni na hiyo ni kutokana na wingi wa matapeli nchini

“Bado watu wengi hawana imani na online business, haswa pale inapokua ni kitu kipya, tofauti na vyakula vyengine kama biriani au fast foods hii inakua ngumu sana kupata order na biashara kutokukua kwa kasi iliyotarajiwa,” anasema

Vipi kuhusu faida

Anasema akiachana na faida anazozipata kwa mfumo wa fedha, Fruitbox Tanzania inamsaidia kukutana na watu tofauti ambao huwa wana mchango chanya kwenye maisha yake binafsi.

“Pamoja na hayo niwaombe tu vijana wenzangu, tulivyokuwa wadogo, tuliambiwa, "watoto ni taifa la kesho" hivyo basi, kesho yetu imewadia, tuchague njia sahihi ya kuijenga zaidi leo yetu kama vile kuwa na marafiki wanaoendana na malengo yako binafsi na kutochagua kazi. Life ia full of surprises, surprise it,” anasema

Nini anapenda

Anasema “Napenda kufanya voiceover na ni kitu ambacho nafanya in my free times au fursa inapotokea. Photography na cinematography pia kwa ajili ya kuandaa contents,” anasema

Aidha anasema kuwa tumaini langu hapo baadae afanikiwe katika kila jitihada anazozifanya hasa ya kuwa mfanyabiashara mkubwa Duniani, kiongozi na mwanamke mwenye misingi bora katika familia.

“Pia mimi nawapenda sana Cher na Jokate, katika upande wao wa harakati za mwanamke, uongozi na upambanaji, kama ni personality ninazotamani niwe nazo, ni zao. Naamini zitanijenga kuwa mtu ninaetamani kuwa na kwa kudra zake Mwenyezi Mungu, nitakuwa,” anasema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post