Palmer Awafunika Foden, Haaland EPL

Palmer Awafunika Foden, Haaland EPL

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer ameshinda tuzo ya kinda bora wa msimu katika Ligi Kuu ya England kwa msimu wa 2023/2024.

Palmer (22) amewapiku Phil Foden, Erling Haaland wote wa Manchester City, Alexander Isak (Newcastle United), Kobbie Mainoo (Manchester United) William Saliba, Bukayo Saka wote wa Arsenal na Destiny Udogie wa Totenham Hotspur.

Staa huyo ambaye ndiyo msimu wake wa kwanza tangu atue Chelsea akitokea Manchester City amefunga mabao 22 na pasi 10 za mabao na kuiwezesha timu yake kujihakikishia nafasi ya kucheza Europa msimu ujao.

Palmer yupo katika nafasi ya pili katika vita ya ufungaji EPL msimu huu akitanguliwa na Haaland wa Man City mwenye mabao 27.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags