Osimhen Aitamani Chelsea

Osimhen Aitamani Chelsea

‘Straika’ wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, amepanga kukataa ‘ofa’ za Paris St-Germain na Saudi Arabia ili ajiunge na Chelsea katika dirisha lijalo.

Osimhen anaripotiwa kuwa na ndoto ya kutaka kujiunga na Chelsea kwa muda mrefu na amevutiwa zaidi na ‘ofa’ yao.

Moja kati ya maeneo ambayo Maurico Pochettino kabla ya kuondoka alisisitiza kwamba anataka yafanyiwe maboresho ni lile la ushambuliaji na jina la Osimhen ndio likawa juu katika orodha ya washambuliaji anaowahitaji.

Licha ya kuondoka kwa #Pochettino, #Chelsea bado inataka kumsajili #Osimhen ingawa ili kufanikisha mchakato huo itatakiwa kuuza baadhi ya wachezaji.

#Napoli inahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni kwa timu yoyote inayomhitaji lakini lengo la staa huyo ni kutua #Chelsea tu na si vinginevyo. Msimu uliopita #Osimhen amecheza mechi 31 za michuano yote na kufunga mabao 17.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags