Omarion: Siwezi kuwa kwenye mahusiano na mwanamke mmoja

Omarion: Siwezi kuwa kwenye mahusiano na mwanamke mmoja

Ooooiii! Wiki ni kama imeanza kibabe hivi, wacha tuulizane kidogo hivi ulishawahi kutana na mwamba kuwa na mpenzi mmoja kwake ni mtihani na hawezi labda kutokana na muonekano wake.

Sasa bhana staa wa nyimbo za RNB kutoka nchini Marekani Omari Ishmael Grandberry maarufu kama Omarion amefunguka na kuleza hawezi kuwa  kwenye mahusiano na mwanamke mmoja kwasababu anagombaniwa sana na wanawake.

"Sifati tamaduni za mahusiano za kizamani kama watu wengine, mwanamke mmoja hanitoshi mimi kwa mtindo wangu wa maisha, kuna ushindani mkubwa wa wanawake wanaotaka kuwa na mimi, so siwezi kuwa na mwanamke mmoja" alisema  Omarion

Hahahahah! Make hapa kwanza ncheke, haya vipi kwa upande wako mtu wangu wa nguvu unaweza kufanya kama mwamba huyu au tukuache kidogo, dondosha komenti yako hapo chini utueleze kuhusiana na mtazamo wako katika hili!!!.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post