Offset na Cardi B wafuta urafiki

Offset na Cardi B wafuta urafiki

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Offset na mkewe Cardi B wamezua gumzo mitandaoni baada ya wawili hao kufuta urafiki kwenye mtandao wa Instagram.

Baadhi ya mashabiki wa wapenzi na wanamuziki hao wamegundua tukio hilo siku ya jana huku sababu ya kufikia uamuzi huo bado haijajulikana, licha ya wanandoa hao siku za hivi karibuni kudaiwa kusalitiana.

Offset na Cardi B walifunga ndoa mwaka 2017 na wamefanikiwa kupata watoto wawili Kulture Kiari Cephus mwenye umri wa miaka mitano na Wave Set Cephus mwenye miaka miwili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags