ODINGA: Nilikwenda Zanzibar kuondoa mshtuko wa uchaguzi

ODINGA: Nilikwenda Zanzibar kuondoa mshtuko wa uchaguzi

Oooooooooh! It’s another furahi day mwanangu sana na kama kawaida yetu tunakusogezea mastory mbalimbali. Basi bwana kiongozi wa Chama cha Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya, Raila Odinga alirejea nchini kimyakimya jana Alhamisi ambapo alikuwa safarini kwa wiki moja.

Akizungumza mjini Mombasa, Odinga alisema alikuwa amesafiri hadi kisiwa cha Zanzibar pamoja na familia yake ili "kupona kutokana na mshtuko" kutokana na kipindi kigumu cha uchaguzi.

“Nilikwenda kupata nafuu katika visiwa vya Zanzibar, nikamchukua mke wangu, watoto na wajukuu zangu pia ili kwenda kuponywa kutokana na mshtuko walioupata kama familia. Tumefika asubuhi ya leo kutoka kisiwa cha Spice Zanzibar na ndiyo maana hatukuweza kuwa nanyi wakati wa kuapishwa,” amesema Raila Odinga.

Aidha ameyazungumza hayo kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Shariff Nassir kufuatia hafla ya kuapishwa kwake.

Ikumbukwe tuu Raila Odinga aligomea mualiko ambao alipatiwa na rais mteule William Ruto na kusema kuwa yuko nje ya nchi na hatoweza kufika katika uapisho huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags