Odinga apanda daladala akielekea kazini

Odinga apanda daladala akielekea kazini

Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga mapema leo Jumatatu, Julai 10, 2023 ametumia usafiri wa umma maarufu matatu nchini humo wakati akienda kazini.

Kabla na baada ya kupanda kwenye matatu, Odinga amesalimia na abiria wenzake na wengine wakionekana kumshangaa na kuzungumzana naye maneno mbalimbali.

“Nikiwa kwenye usafiri rahisi na rafiki wa umma nikielekea kazini asubuhi ya leo,” ameandika Odinga.

Ndani ya usafiri huo uliokuwa ukipitia barabara ya Ngong-Nairobi, wapiga debe wakilalamikia gharama ya juu ya mafuta. Abiria wengine walimweleza kuhusu gharama ya juu ya maisha, wakisema nchi haiendi kwenye mwelekeo sahihi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags