Wakati mashabiki wakikoshwa na kazi za muziki kutoka kwa Ahmed Ololade ‘Asake’ kufuatia na mtindo wake wa uimbaji kwenye Afrobeat, Afropop, na Amapiano, nyuma yake yupo mwanadada ambaye ni meneja wake aitwaye Alexa Rae Perkins.
Alexa ni mtaalamu wa usimamizi wa wasanii na huduma za ubunifu katika kampuni ya EMPIRE, mwanadada huyo anadaiwa kuwa meneja wa Asake wa sasa baada ya wawili hao kuonekana pamoja katika matamasha mbalimbali Marekani.
Ikumbukwe mwanadada huyo aliwahi kushiriki picha ya pamoja na Asake kwenye ukurasa wake wa Instagram wakati wa hafla ya Tuzo za Grammy huku akimpongeza kwa kipaji chake kinachowavuruga wengi, na kumuita mshirika wake katika biashara.
Mbali na wawili hao kudaiwa kufanya kazi pamoja lakini baadhi ya vyanzo vya karibu vinadai kuwa wawili hao huwenda wana uhusiano wa kimapenzi.
Endapo Alex atakuwa meneja wa Asake basi atachukua nafasi ya meneja wa msanii huyo aitwaye Stephen "Sunday" Are, ambaye pia amewahi kufanya kazi na wasanii wengine wakubwa kama Wizkid.

Leave a Reply