Nyota wa ‘Pirates of the Caribbean’ afariki dunia

Nyota wa ‘Pirates of the Caribbean’ afariki dunia

Mwigizaji kutoka Marekani aliyefahamika zaidi kupitia filamu yake ya ‘Pirates of the Caribbean’ Tamayo Perry amefariki dunia baada ya kuliwa na samaki aina ya Papa.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na Meya kutoka jimbo la Honolulu, Rick Blangiardi akiweka wazi kuwa kifo cha mwigizaji huyo kimetokea eneo la ‘Malaekahana Beach’ ambapo alikwenda kwa ajili ya kuogelea, huku akisikitishwa na kumpoteza mtu mahiri katika jimbo hilo.

Mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 49, ambaye alikuwa mtaalamu katika uokoaji, alifariki Dunia baada ya kufikishwa nchi kavu na waokoaji wenzake.

Enzi za uhai wake Perry, alijishughulisha na uwalimu wa uimbaji, uigizaji na mpenzi wa kuogelea jina lake lilijulikana zaidi katika filamu kama ‘Pirates Of The Caribbean: On Stranger Tides’, ‘Blue Crush’, ‘The Big Bounce’, ‘Six Days in Paradise’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags