Nyota wa mchezo wa ‘Ice-Hockey’ afariki uwanjani

Nyota wa mchezo wa ‘Ice-Hockey’ afariki uwanjani

Mchezaji wa kulipwa wa mchezo wa ‘Ice-hockey’ kutokea #Marekani #AdamJohnson mwenye umri wa miaka 29, amefariki dunia jana usiku kwa ajali ya kukatwa shingo na fimbo inayotumika kupigia mpira (kitufe).

Ajali hiyo ilitokea wakati wa ‘mechi’ ya Derby kati ya ‘timu’ yake ya #NottinghamPanthers na #SheffieldSteelers iliyokuwa ikichezwa huko Sheffield nchini Uingereza.

Wachezaji wa ‘timu’ zote mbili walimzunguka mwenzao na kumsitiri wakati akipatiwa huduma ya kwanza.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo inadaiwa kuwa ‘mechi’  ilisimamishwa na mashabiki takribani 8,000 waliamriwa kuondoka uwanjani na ‘mechi’ zote za mcezo huo zimeahirishwa.

Adam amewahi kucheza ‘timu’ mbalimbali zikiwemo Pittusburgh Penguins, Malmo Redhawks , Ontario na Augsburger Panther.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags