Nyota Wa Kwenye Spider-Man, Achumbia

Nyota Wa Kwenye Spider-Man, Achumbia

Jacob Batalon ambaye alipata umaarufu kupitia filamu ya Spider-Man, akicheza kama Ned Leeds amemchumbia mpenzi wake wa muda mrefu Veronica Leahov.

Tukio la wawili hao kuchumbiana limeibua mijadara katika mitandao ya kijamii wakieleza kuwa huwenda kukawa na harusi mbili kwa wakati mmoja mwaka huu baada ya Tom Holland kumchumbia mpenzi wake Zendaya miezi michache iliyopita.

Jacob Batalon na Tom Holland wameonekana pamoja kwenye filamu kutoka kampuni ya Marvel Cinematic Universe (MCU), Spider-Man: Homecoming (2017), Avengers: Infinity War (2018), Avengers: Endgame (2019), Spider-Man: Far From Home (2019) na Spider-Man: No Way Home (2021).

Katika filamu hizo Tom Holland anaigiza kama Peter Parker/Spider-Man, huku Jacob Batalon akiigiza kama Ned Leeds, rafiki yake wa karibu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags