Nyota wa Harry Potter afariki dunia

Nyota wa Harry Potter afariki dunia


Mwigizaji wa Uingereza Dame Maggie Smith ambaye alijulikana zaidi kupitia mfululizo wa filamu ya ‘Harry Potter’ amefariki dunia asubuhi ya leo Septemba 27, 2024 akiwa na umri wa miaka 89.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na watoto wake Toby Stephens na Chris Larkin wakieleza kuwa mama yao alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu hoispitali.

"Alifariki kwa amani hospitalini mapema asubuhi ya leo, Ijumaa tarehe 27 Septemba, ameacha watoto wawili na wajukuu watano ambao wamevunjika moyo kutokana na kifo. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wafanyakazi wa Hospitali ya Chelsea na Westminster kwa huduma na wema wao wa hali ya juu wakati wa siku zake za mwisho." Imesema taarifa hiyo

Hata hivyo watoto hao hawajaweka wazi sababu ya kifo cha mama yao huku wakiwaomba mashabiki kuwapatia faragha kwa sasa.

Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar anafahamika zaidi kwa uhusika wake kwenye filamu maarufu zilizotokana na mfululizo wa vitabu vya J.K. Rowling, ambapo stori za kwenye vitabu hivyuo ziliamishiwa kwenye filamu iitwayo Harry Potter and the Sorcerer's Stone mwaka 2001.

Enzi za uhao wake ameonekana katika filamu kama The Miracle Club, Nanny McPhee Returns, Sister Act, Ladies in Lavender, A Boy Called Christmas, Downton Abbey: A New Era na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags