Nyimbo Za Kutendwa Zasikilizwa Zaidi Msimu Huu Wa Valentine

Nyimbo Za Kutendwa Zasikilizwa Zaidi Msimu Huu Wa Valentine

Msimu wa Valentine mara nyingi husindikizwa na nyimbo za mapenzi na zilizojaa mahaba duniani kote. Lakini kwa mwaka 2025 imekuwa tofauti Barani Afrika kwani panatajwa kusikiliza zaidi nyimbo za kutendwa ‘Heartbreak Song’.

Kwa mujibu wa takwimu za Spotify, nyimbo za ‘heartbreak’ zilipata ongezeko kubwa la streams huku orodha hiyo ikiongozwa na nchi ya Nigeria ambayo ilipata wafuatiliaji (626%), Ghana (226%), Uganda (206%), Kenya (189%), na Tanzania (132%).

Hata hivyo katika orodha hiyo imewataja wanaume kuwa wanaongoza zaidi kusikiliza nyimbo hizo. Ambapo wanaume wana asilimia 52 na wanawake asilimia 46, huku hatua hiyo imeripotiwa kupinga dhana kwamba wanawake pekee ndio wanatafuta faraja kupitia muziki wa kuumiza.

Takwimu za Spotify pia zinaonyesha kuwa nyimbo za ‘heartbreak’ hupata idadi kubwa zaidi ya wasikilizaji kati ya saa 10 jioni na saa 12 jioni, muda unaoendana vyema na safari za kurudi nyumbani kutoka kazini na mapumziko ya jioni.

Aidha kufuatia na chapisho hilo wataalamu wanasema muziki ni tiba kwa walio na maumivu ya mapenzi ambapo watu wengi wanapenda kusikiliza nyimbo hizo kwa ajili ya kupona majera na kutulia maumivu waliyoyapa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags