Nuh Mziwanda :Nifungulie nateseka

Nuh Mziwanda :Nifungulie nateseka

Aisee hii siyo ya kwaida bwana ambapo msanii wa bongo fleva  Nuh Mziwanda ameamua kutupa jiwe gizani baada ya kutoa dukuduku lake moyoni kwa kuomba afunguliwe alipofungwa .

Kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram Nuh Mziwanda ameandika ujumbe huu "Sipendi bifu wala ugomvi ndio mana napenda sana amani na kuongea ukweli wa Moyo wangu bila kujali mtu mwingine atanichukulia vipi, ila ukiona unataka amani na bado mtu ana vita ya kukudidimiza ujue unaelekea kwenye unyonge na kuonewa huruma kama Ukraine".

"Naomba kanifungue niwe free tena kama zamani, usinifungie nateseka sana nina familia yangu inanitegemea na sihitaji mapenz na wewe nahitaji ukanifungue tu

Ebwana eeeh!!! Unafikiri dogo hili amemtupia nani? Dondosha comment yako chini kupitia www.mwananchiscoop.co.tz.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags