Njia za kuposti video, picha bila kupoteza ubora wake

Njia za kuposti video, picha bila kupoteza ubora wake

Watu wengi wamekuwa wakichukizwa na matokeo wanayopata baada ya kuposti picha au video kwenye mtandao wa Instagram kutokana na wanachoposti kupungua ubora wake wa mwanzo.
Hivyo basi hizi ndiyo njia za kusaidia video na picha zako kutopungua ubora mara baada ya kuposti.

1, Katika akaunti yako ya Instagram upande wa kulia bonyeza mistari mitatu midogo inayoonekana.

2, Baada ya kufanya hivyo itakuletea machaguo mengi, bonyeza sehemu iliyoandikwa Settings and Privacy.

3, Mara baada ya kubonyeza Setting and Privacy chagua sehemu iliyoandikwa Data usage and Media quality.

4, Moja kwa moja itakupeleka katika machaguo mengine hakikisha unawasha kitufe cha Upload at highest quality.
Na hiyo itakuwa ndiyo hatua ya mwisho ya kufanya uweze kuposti picha na video bila ya kupoteza ubora wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post