Njia za kuongeza ubunifu katika kazi

Njia za kuongeza ubunifu katika kazi

Niaje mtu wangu!! leo kwenye makala ya kazi, ujuzi na maarifa nimekuzogezea mbinu ambazo zinaweza kukusaidia kuongeza ubunifu katika kazi yako.

Twende sawa njia hizi kila mtu anaweza kuzitumia lakini sana sana ni kwa viongozi ili kuongeza ubunifu binafsi na wale wanaofanya nao kazi.

Tengeneza mazingira na mbinu ya kufanyia kazi mawazo yako ya kibunifu na yale ya wale unaofanya nao kazi.

Kuwa na mawazo ya kibunifu ni jambo jema lakini kuishia kua na mawazo ya kibunifu ni kazibure, ni lazima kazi ya ziada ifanyike ya kutengenenza mazingira kwa ajili ya kuanza fanyiakazi hayo mawazo ya kibunifu yaliyopatikana, unapokua umefanya uchunguzi yakinifu juu ya uwezekano wa kufanikiwa na kiutendaji wa wazo bunifu ni muhimu sana kuamua kuanza wekeza muda na rasirimali katika kuanza kulitendea kazi wazo hilo la kibunifu .

 Pale watu unaofanya nao kazi wanaona mawazo yao ya kibunifu yanafanyiwa kazi itawapa hamasa zaidi ya kuzidi kua wabunifu zaidi na hii huchipua ufanisi katika kazi.

Fanya maamuzi kwa kushirkishana na kuulizana na si kuamrishana

Watu wengi walio wabunifu hawapendi kuamrishwa sana, hupenda kufanya vitu kufuatia kusudio na kwa ridhaa ya mioyo yao. Na katika mazingira ya kazi hii lazima ianze kuwa tabia ya viongozi haswa wa juu na kama kiongozi ni muhimu sana kuwahamasisha uwaongozao kujenga tabia ya kutokuamrishana bali kuelekezana majukumu kwa njia ya kistaarabu issyo mfanya mwingine kujihisi kunyimwa uhuru wa kuchagua na kuamua na waonapo wewe kiongozi wajuu unaishi taratibu hiyo mpya hata wao watavutika kuiishi na hata kupelekea ubunifu kuongezeka na hivyo ufanisi.

Jenga misingi ya kuaminiana na kuheshimiana baina ya viongozi wakubwa na wafanyakazi wa kawaida.

Mawazo bora ya kibunifu huweza tokea kutoka kwa mtu yeyote pasipo kuzingatia hali yake, elimu yake ma cheo chake, hivyo ni muhimu misingi ya kuheshimiana na kuaminiana ikajengeka ili kuruhusu wafanyakazi wote kua huru kuelezea mawazo yao katika hali ya kujiamini mbele ya watu wote na kuyafanyia kazi yote pasipo ubaguzi kwani hii itachangia ushirikiano na kujenga hali ya kujiamini na kujaribu zaidi hata kuchipua uwezo wa kibunifu ndani ya wafanyakazi wote ,hii huleta ufanisi katika kazi.

Futa tamaduni ya kushindikana kwa mawazo

Watu wengi sana ubunifu wa mawazo yao umepotea hivi hivi kutokana na hali ya kujiaminisha kua mawazo yao hayawezekani kwa sababu wanazoziiita zipo nje ya uwezo wao, hivyo ile hofu ya kushindikana kwa mawazo kumepelekea kuua uwezo wa kibunifu wa watu wengi, na hii inadhihirika katika kuogopa maneno ya watu wengine ikiwemo kebehi, dharau na vicheko.

Na njia pekee ya kuiiondoa hii tamaduni ni kuwajenea wafanyakazi wako uhakika wa kufaulu na kushindwa kwa mawazo yao na kuwahakikisha wote wanaelewa mchango wa kushindwa katika kuja na mawazo bora zaidi ya kibunifu, Kushindwa ni moja ya njia muhimu sana kuanzisha na kuendesha biashara yeyote na kila kushindwa huleta mafunzo muhimu sana ambayo huchangia kuongeza ufanisi katika kazi.

Teneneza mazingira ambayo mawazo yaliyoshindwa hayatazungumziwa katika vikao vya thathmini vya kikazi ama kuhuishwa katika utoaji wa fidia na kuishi na tamaduni kua njia pekee ya kua mbunifu zaidi ni kushindwa zaidi na kutafuta namna ya kuboresha utendaji wa pale paliposhindikana kwani hata watu wabunifu sana hukosea mara nyingi tu.

Hivyo kumbuka kuwa ni kupitia ubunifu pekee ukuaji wa biashara na maendeleo huja na kupitia ubunifu pekee ufanisi.

I hope tutakuwa tumefahamiana vizuri zingatia hayo ili uweze kufanya kazi zako vizuri na wenzako nakutakia jumatatu tulivu kabisaa!


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post