Njia za kudhibiti strees chuoni

Njia za kudhibiti strees chuoni

Niajeee! Wanangu wa vyuoni, sikukuu inasemaje pande hizo, vipi mmeshapata maabaya au sio shida zenu, oky tuachane na hayo, kuna msemo unasema kuwa chuo hakuna strees nyie nyie hili jambo lisikieni tuu. kuna watu wanapata tabu sana ila hatujui.

Kama mnavyojua watu wengi wanaficha sana madhaifu yao akiwa mbele za watu atacheka na nyie lakini moyoni mwake mungu mwenyewe ndo anajua, sasa leo nikaona nizungumze na watu hawa ili kujua namnagani tunawasaidia.

Chuo kuna mambo mengi sana ya kutia strees ukisema uyatilie maanani basi yatakuumiza kila siku na kuna yale mingine ni yakipuuzi kabisa mfano mtu kuwa na strees ya kujaji mwonekano wake au kutaka kuishi maisha ambayo sio yake kupritend maisha, haya ni mambo ya kipuuzi na sio ya kuyaweka kichwani.

Leo hapa nazungumzia zile strees ambazo mtu anakumbana nazo katika masomo yake, familia, maswala ya kifedha, kuwaza kuhusu kupata kazi nk. Kwanza kabla hatujaanza kuelezana chakufanya ni kujua unachoweza kufanya ili kuondoa strees na wasi wasi.

Mfano mimi huwa nikiwa na strees najifungia ndani na kuangalia move sometime naamua kulia tuu, kuna watu wanasemaga kulia kunaweza kukusaidia kuondoa machungu yote yaliyo moyoni so ni wewe kujua nini ukifanya kinaondoa strees zako.

Hizi ndo baadhi ya njia za kudhibiti strees ulizo nazo chuoni, na si chuo tuu hata kwa mtu wa kawaida

  • Kufanya mazoezi

Kama unataka kupunguza strees ulizo nazo cha kwanza inabidi ujizoeshe kufanya mazoezi unahitaji tu kufanya moyo wako kwenda mbio, kwa mfano kwa kutembea haraka haraka au kuendesha baiskeli itakusaidia sana kupunguza yamoyoni mwako.

  • Kuzungumza na watu

Kujitenga kunaweza kuwa na athari mbaya sana kwenye furaha yako. Kukubali kwamba unahitaji msaada na kuzungumza na mtu mara nyingi ni hatua ya kwanza ya kujisikia vizuri.

Ongea na marafiki na familia yako - wanakujua vyema na wanajali zaidi kukuhusu. Zaidi ya hayo, tafiti zinaonyesha kuwa kushirikiana na rafiki mara moja tu kwa wiki kunaweza kupunguza viwango vyako vya mfadhaiko na kuboresha hali yako kama vile matibabu au ushauri.

Ongea na wanafunzi wengine kwenye kozi yako na labda utapata kuwa hauko peke yako. Hii inaweza kusaidia kuweka mambo katika mtazamo. Waulize ni mbinu gani wanazotumia kudhibiti strees zako.

  • Kupata usingizi wa kutosha

Hii inaweza kuonekana kama suluhisho dhahiri lakini mara nyingi hupuuzwa. Afya yako ya akili na ustawi hutegemea wewe kupata usingizi wa kutosha, kwani hakuna mtu anayefanya kazi kwa 100% akiwa amechoka.

Jaribu kuamka na kwenda kulala kwa wakati mmoja kila siku. Saa saba hadi nane za kulala zinapendekezwa. Hili linaweza lisiwe halisi kila usiku wa wiki lakini lenga kufikia lengo hili mara nyingi zaidi.

  • Ondoa mawazo yako mbali nayo/jufunze kumanage strees zako.

Fanya kitu unachofurahia na kitakachokusumbua kwa muda kama vile kusikiliza muziki, kusoma, kuoka mikate au hata kushona nguo zako zilizo chanika, jipe majukumu na kazi mbalimbali kuondoa strees zako.

Kula kwa afya na kula vyakula vipya. Badilisha mawazo yako na uwe na mtazamo chanya. Punguza kutumia social media kwasababu sinaweza kukumbusha kwa yale unayo yapitia. 

Kucheka, tumia wakati na rafiki wacheshi, tazama kitu cha kipuuzi au uweke kitabu cha simulizi za vichekesho au kwenda katika sehemu wanazofanya matamasha ya vichekesho kama vile cheka tu, watubaki nk. Hii itakusaidia sana kupunguza msongo wa mawazo ulionao.

Iwapo umejaribu mbinu hizi zote za kukabiliana na hali hii lakini hauwezi kushinda mzunguko wa mfadhaiko, ni wazo nzuri kumtembelea daktari ili kuangalia kwamba dalili ulizo nazo zinahusiana na mfadhaiko au kuna tatizo jingine.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post