Hellow! Niaje niaje wanangu sana tunaendelea tulipoishia bwana maana, hatuwezi kusomesha maneno elfu moja lazima tuende kidogo ili tuweze kuelewana bwana.
Tulipo ishia ndo tunapoendelea kama kawaida, bwana hakuna maisha maguma kama ukimaliza chuo halafu ukose kitu cha kufanya yani upo upo tuu nyumbani, tena kipindi hichi bwana hadi marafiki wanakutenga kabisa yaani.
Sasa ili usiwe mpweke nyumbani, wala kukosa marafiki njia mpya ya kupata marafiki baada ya kumaliza chuo ili uweze kuchangamana na watu na hapa hatuzungumzii marafiki wa kwenda nao kidimbwi ni wale watu wakukufanya ufanikiwe au kwa maana nyingine kukufungulia dunia yako mpya ya mafanikio.
- Ongeza mitandao ya kijamii/ jua kutumia mitandao yako ya kijamii vizuri
Hatua nyingine nzuri ya kupata marafiki baada ya chuo ni kutumia vyema mitandao yako ya kijamii. Utahitaji marafiki karibu nawe kila wakati, haijalishi ni nini kinaendelea katika maisha yako.
Siku hizi bwana technology inatusaidia sana kujulikana so unachotakiwa kukifanya katika mitandao yako ya kijamii usiposti mambo ya ajabu ajabu ila zile ambazo unaonekana uko serious mfano picha ulizopiga katika kusaidia watu au event mbalimbali nk.
Kushiriki katika shughuli unazofurahia ni njia nzuri ya kukutana na watu wapya. Kwa usaidizi wa mbinu hii, utaweza kuungana na wengine wanaoshiriki mambo unayopenda na kuendeleza shughuli.
Kulingana na mambo yanayokuvutia na mambo unayopenda, tafuta mtandaoni kwa kikundi ambacho kinashiriki mambo yanayokuvutia. Kisha, wasiliana mtandaoni na upange mikutano ya live kuendelea kufuatiliwa na wafuasi wako.
Toa maoni kwenye posti za watu wengine, sio watu wengine tuu bali ni watu wenye wadhifa kidogo.
- Hudhuria makongamano tofauti tofauti
Kwanza embu tuulizane kidogo hivi umewahi kwenda kwenye tukio na kujikuta ukiingia kwenye chumba kilichojaa watu usiowatambua yaani unaona kila mtu anakutazama wewe hahaha! Usiombe ikukute lakini hata ikikukuta itakusaidia kuwa jasiri Zaidi mbele za watu.
Nikizungumzia makongamano nasemea yake ya kiserikali ama yale ya kibiashara
Haijalishi ni aina gani ya lengo unalojaribu kufikia, iwe ni kwa ajili ya maisha yako ya kibinafsi, biashara yako, au maisha yako ya kijamii; malengo yana nguvu sana.
Hii ni mojawapo ya njia bora za kupata marafiki baada ya chuo kwasababu mfano ukaenda katika makongamano ya kiserikali utaweza kujuana na watu wakubwa mnaweza kubadilioshana namba huwezi jua ipo siku itakusaidia sana.
- Kutana na Marafiki wa Marafiki zako
Hii ni mbinu nzuri ya kukutana na watu wapya! Jitihada nyingi za kiakili zinaweza kuokolewa kwa kutumia miunganisho iliyopo badala ya kuchukua hatua ya kwanza inapokuja suala la kuunda urafiki mpya.
Kubali mialiko ya rafiki yako kwa hafla na shughuli pamoja na marafiki zake, kama tunavyojua kuwa mtu ambaye ni rafiki wa rafiki yako ni rafiki yako pia.
Hii itakusaidia sana katika kukuza fikira yako kwa kupata mawazo mapya kutoka kwao, pia kupitia wao ukapata mialiko ya event mbalimbali ambazo zina hadhi na kukufanya kujulikana na watu wakubwa Zaidi.
Swali ambalo wengi hujiuliza ni kwa nini ni vigumu kupata marafiki katika miaka yako 20
Ni vigumu kukutana na watu wapya katika miaka yako ya 20,21,22 nk kwasababu watu wengi watakuchukulia bado hujakua na akili yako bado haijatengemaa katika kufikiria mambo mengine mfano kufikiria maisha yako ya baadae ndo maana ni ngumu sana kupata rafiki mpya kwa miaka yako, kila mtu anakuona bado hujakua kiakili.
Anachojua kwako kuwa ratiba yako kila siku ni ile ile ulioizoea ukiamka asubuhi uende chuo urudi nyumbani nk, mfanye mtu akuamini kuwa umekuwa jiweke mwonekano ambao hata kama unamapungufu mtu asiweze kukujua hapo kwa hapo itakusaidia sana katika kupata marafiki ambao watakusaidia kufanikiwa kimaisha.
Okey okey tufanye kama tumemaliza hivi lakini cha muhimu sana ni kuacha kulala ndani kusubiria sehemu uliopeleka barua ya kuomba kazi ili uweze kujibiwa, amka sasa na uanze kuchangamana na wenzio ambao wanamawazo tofauti na yako itakusaidia sana kuliko kubaki nyumbani, kubali kuonekana mjinga kwa kujitolea katika ofisi yoyote ile usiangalie nimesomea kitu Fulani kwahiyo lazima nipate kazi sehemu fulani, siku hizi msemo wetu ni kazi kazi ilimradi mkono uende kinywani.
MWISHOOOOOOO!
Leave a Reply