Njia wanayotumia wazazi China kuwatafutia watoto wao wenza

Njia wanayotumia wazazi China kuwatafutia watoto wao wenza

Wakati baadhi ya wazazi wa Bongo wakiwatafutia watoto wao wenza katika familia zenye uwezo ama ambazo wanajuana nazo kwa muda mrefu, lakini jijini Shanghai nchini China ni tofauti kabisa kwani wazazi hupeleka CV za watoto wao katika soko unaofanyika kila wiki.

Jiji la Shanghai, katika eneo la People's Park siyo tu mahali tulivu pa kucheza chess na kutembea na mbwa bali ni sehemu pia ya kutafutia mchumba ambapo kila mwisho wa wiki katika bustani hiyo kunageuka sehemu ya watu kutafuta mume/mke ambapo baba na mama ndio wanafanya hivyo kwa niaba ya mtoto wao.

Katika mnada huo jukumu la wazazi linakuwa ni kuwapigia debe na kuwanadi watoto wao mfano wa kuomba kura huku wakiambatanisha na vitu vya mtu husika ikiwemo umri, urefu, Chuo alichosoma, Kazi anayoifanya, Biashara alizonazo, Watoto, Thamani anazomiliki nk.



Soko au mnada huo ujiulianzishwa mwaka 1996, kwa ajili ya wazazi haswa wakiume kuwasaidia watoto wao ambao hawawezu kupata wenza (hawawezi kutongoza) kufanikisha waweze kupata wenza kabla hawajafikisha miaka 30.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags