Njia rahisi za kusoma na kufaulu

Njia rahisi za kusoma na kufaulu

Yawezekana unasoma sana mtu wangu wa nguvu lakini matokeo yakitoka hutamani rafiki au hata wazazi wako wajue kile ulichopata katika mitihani yao hasa ile ya mwisho.

Au unafanya vizuri darasani na mitihani ya kawaida lakini inapofika muda wa kufanya mitihani ya mwisho kama vile ya wilaya, mkoa na taifa unafeli mpaka unahisi unafanyiwa hila au umelogwa!

Kufeli sio jambo zuri kwa mtu kulipata katika kitu chochote hasa ukiwa chuoni, kwa kutambua hilo haijalishi wewe ni mwanafunzi wa chuo gani na hadhi gani au unarudia mtihani huna budi kujua njia hizi rahisi sana za kukusaidia kufaulu mitihani yako.

Zifuatazo ndio njia hizo nakusihi sana wewe mwanafunzi zisome kwa makini….

  1. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOLISOMA

Kujua topic za kila somo unalotarajia kujibu mtihani wake kutakusaidia sana kujua mada zipi huwa na maswali mengi, alama nyingi na zile zenye maswali rahisi na magumu.

Hii inakupa mwongozo sahihi sana wa kujua wapi pa kuanzia pindi unavyojiaandaa kujibu mtihani. Ni hatari sana kuingia kwenye chumba cha mtihani ukiwa hujui maswali yapi ya kuanza kwenye mtihani husika hata kama unajua vitu vingi vya kujibu.

  1. SOMA MITIHANI ILIYOPITA

Njia hii ni rahisi sana itakusaidia kujua namna ya kujibu maswali, kujua mitego na mbinu za watunga mitihani ambao mara nyingi hurudia maswali yaleyale kwa namna tofauti.

Vilevile itakusaidia kujua format au miundo ya mitihani na hii itapelekea wewe kujua majibu ya maswali mengi sana ndani ya muda mfupi sana.

  1. SOMA KWA MALENGO

Kusoma sio hekali za shamba unazotakiwa kutumia muda mrefu sana ili umalize kuzilima la hasha ! kusoma ni kazi inayohusisha akili na viungo hivyo unatakiwa kuwa na lengo maalumu kila unaposoma sio kusoma ilimradi.

Ni heri ulale upumzishe akili kuliko kusoma ukiwa hauelewi kitu husika unachokisoma kina faida gani kwako. Ndio maana wapo baadhi ya wanafunzi wanaotumia muda mrefu hufeli wakati wapo watu wanaofaulu licha ya kutoingia darasani wala kusoma muda mrefu.

Hii ni kwa sababu wengi wa wanafunzi wanaosoma muda mrefu husoma bila ya kujua lengo la kusoma vitu au mada fulani na kuishia kufeli.

  1. TUMIA MUDA MWINGI KUSOMA MASOMO UNAYOYAELEWA VIZURI.

Kutumia muda mwingi kwenye masomo unayoyaelewa vizuri haimanishi uache kusoma masomo mengine,ila hii ina maana kwamba unatakiwa kuelewa zaidi na zaidi na kugeuza masomo yote unayoyaelewa kama uwanja wa nyumbani kiasi kwamba katika mitihani ya masomo hayo unakuwa na uhakika wa kupata zaidi ya 65% mpaka 75% .

Mbinu hii ni rahisi sana na muhimu maana ufaulu hutegemea alama za masomo tofauti tofauti na sio somo moja tu. Hivyo jua zaidi kwenye masomo unayoyaelewa yatakulipa kwenye mitihani na kukupa uhakika wa kufaulu.

  1. SOMA NOTES FUPI ZENYE KUBEBA MAWAZO YA MSINGI

Badala ya kusoma maelezo mengi kama msomaji wa risala, notes fupi zilizo andaliwa vizuri zitakusaidia kufaulu mtihani kirahisi. 

Njia hii itakusaidia kutokuishiwa hamu ya kusoma unapotumia notes fupi, husaidia kuelewa haraka na kwa mujibu wa wataalamu wanadai notes fupi husaidia sana kumtunzia mwanafunzi kumbumbu nzuri.

  1. BUNI KANUNI ZA MAJIBU

Kubuni Kanuni ni ujanja wa aina yake asikudanganye mtu, elewa kwanza hizi sio kanuni rasmi bali ni kanuni ambazo mtu anabuni kwa namna yake akiwa na lengo zimsaidie kutunza kumbukumbu na zimrahisishie anapojibu maswali.






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags