Njia asili za kuondoa weusi makwapani

Njia asili za kuondoa weusi makwapani

Na Aisha Lungato

Hellow natumai ni wazima wa afya bwana leo kwenye urembo na fashion nimewaletea dawa ya lile tatizo sugu linalo waumiza vichwa mabinti wengi

Sasa fahamu jinsi ya kuondoa icho kirangi kwenye kwapa au mapajani tofauti na artificial ways ambazo labda ni gharama, zina madhara au wanaona hazifanyi kazi.Tips zifuatazo ni rahisi sana na zinafanya kazi lakini lazima ufanye kwa muda kidogo ili uanze kupata matokeo angalau wiki mbili kila siku sababu hizi sio kemikali.

1. MAFUTA YA NAZI
Hakuna kitu ambacho mafuta ya nazi hayafanyi!!hata hivyo ni kiungo cha urembo duniani kote.Inafanya kazi taratibu.Hivyo nashauri utumie kila siku. Jisugue (massage) na mafuta ya nazi kwa dakika 15 kabla hujaoga.Wapenzi wa deodorant hii pia ni deodorant ya asili.

2. LIMAO

Hii unaweza kutumia kutoa weuse sehemu yoyote ya mwili,iwe kwenye mapaja au kwapani.Ni rahisi kata kipande cha limao sugua kwapa lako, acha kwa dakika kumi halafu oga. Kumbuka limao inasaidia kutoa harufu mbaya pia kwenye kwapa. Paka mafuta laini au deodorant kuzuia ngozi isikauke.

3. VIAZI MVIRINGO
Hii pia ni bleaching agent kama limao. Lakini viazi ni vizuri zaidi sababu havikaushi ngozi na havisababishi muwasho wowote.Unaweza sugua kwapa na kipande cha kiazi au ukasaga kiazi chako kwa blenda na kujisugua na juisi yake kasha kuoga baada ya dakika kumi.

4. TANGO
Tofauti na kuleta harufu nzuri mdomoni, kuondoa weusi machoni, habari njema ni kwamba ukisugua kipande cha tango sehemu yenye weusi mara mbili kwa siku tatizo hilo huisha.Unaweza tumia na limao au asali kwa pamoja.

5. MAGANDA YA MACHUNGWA
Warembo wangu hii itawafaa, kausha vizuri maganda ya machungwa kwa siku tatu juani.Yatwange au saga kutengeneza poda au ungaunga weka kwa kikopo na funika.Chota vijiko viwili changanya na rose water (inapatikana madukani) paka kwapani. Acha ikauke kwa dakika kumi halafu uoshe na maji baridi. Kwani bafuni tunaweka nini zaidi ya vitu kama hivi? Msimu wa machungwa haujaisha wapenzi.

6. APPLES
Apple ina kiwango cha acid pia hivyo ukisugua kwapa na apple lililosagwa inatoa weusi na harufu. Fanya hivi angalau mara moja kwa siku kabla ya kuoga.

7. MAZIWA
Wapenzi wa kunywa maziwa siwaoni wakifanya hii…ila ina majibu ya haraka ukifanya kila siku. Paka maziwa kidogo tu kwenye kwapa acha yakauke kwa dakika 15 halafu oga. Fanya hivi kila siku kupata majibu.

Haya haya warembo wangu wazuri unaweza kuchagua tips moja na ikakusaidia tumia ambayo unauwezo nayo ondoa hiyo aibu mwarii, usisahau kicomment hapo chini @mwananchscoop






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags