Njia 10 za kufanya nywele zako zivutie na kukua

Njia 10 Za Kufanya Nywele Zako Zivutie Na Kukua

Habari msomaji wa fashion, Ni wiki nyingine tena tunakutaka ili kuelezana na kujuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya mitindo, urembo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua tu zaidi.

Mpendwa msomaji leo hii tutaangalia njia 10 ambazo kama ukizitumia vizuri na inavyotakiwa basi nywele zako zitavutia na kukua.

Watu hawaelewi kuwa kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto ambavyo ni vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu.

Pia vipo aina ya vyakula tunavyokula ambavyo ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako.

Ili nywele yako ikue na kuvutia kwanza kata ncha za nywele zako, kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujijaza upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa.

Seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi.

Lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

 

Pili onya nywele zako angalau mara moja kwa wiki kwani kwa kufanya hivyo angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. Hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuosha nywele zako.

Tatu, tumia shampoo inayoendana na nywele zako, tunajua kuwa kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito.

Zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo, hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie.

Nne, zipe nywele nafasi, watu hawaelewi kuwa nywele nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku,  kuzipaka nywele jeli kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya zichoke na kukosa afya.

Hivyo basi unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kupumzika. zipumzishe nywele zako kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu.

Tano, usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi unachotakiwa ujaribu kuzichana kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane kwani  unapochana zikiwa mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibu ukianzia nyuma kuja mbele.

Aidha kuchana nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

 

Sita, zilinde nywele zako unapokuwa unaogelea, najua wadada wengi wanapenda kuongelea sasa unapokuwa huko baharini au kwenye bwawa la kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzui zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe kwa maji safi na uzikaushe.

Saba, kula vyakula venye protin na matunda kwa kula vyakula hivyo kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

Nane, zifunge nywele zako kabla ya kulala au unaweza kuzisuka mabutu, kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika

Tisa, Tumia mafuta asili, badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka kwenye nywele zako.

Kumi, zilinde nywele zako na jua, wakati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia au mtandio.

 
Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Janeth Jovin

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on business, money management on Tuesday and health on Thursday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include KARIA and FASHION.

Latest Post