Njaa yawatesa wakazi wa Arumeru

Njaa yawatesa wakazi wa Arumeru

Ukosekanaji wa Mvua  baadhi ya maeneo mkoani Arusha yamekumbwa na uhaba wa chakula kutokana na ukame, baadhi ya Wakazi wa Arumeru mkoani humo hasa Wanawake na Watoto wamelazimika kutembea umbali mrefu kuomba Chakula.

Diwani wa Tarafa ya King’ori, Rosemary Mtalo, amesema “Kweli Watu wana njaa ila siyo kwa kiwango kikubwa na hakuna taarifa ya Mtu kufa kwa njaa.

Michakato ya kuwasaidia inaendelea, tumepeleka mapendekezo Serikalini Wananchi wasaidiwe Chakula na tumeshaandika majina ya Kaya.”

Maeneo ambayo yamekumbana na changamoto hizo za ukosefu wa chakula ni Oldonyo Sambu, King'ori, Ngwansio, Malula, Kata ya Ngaramtoni, Kata za Tindigani na baadhi ya Kata za Wilaya ya Hai


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post