NIT mabingwa shimivuta bila kupoteza mchezo

NIT mabingwa shimivuta bila kupoteza mchezo

Habari yako mdau na mfuatiliaji wa magazine ya Mwananchi scoop kama kawa kama dawa ikiwa tumebakiza siku moja kueleekea kwenye sikuu ya Christmas bwana kama ilivyoada Ijumaa hua tunatoka na zile makala za michezo na burudani.

 Ijumaa hii bwana bahati imeangukia katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo wameibuka kidedea baada ya kushiriki kwenye mashindano ya shirikisho la michezo vyuo vya elimu ya juu(Shimivuta).

Yees!! Hivi ndivyo tunaweza kusema bwana na kongole nyingi sana kwa mabvingwa wa Shimivuta kutoka chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT.

Hii imekuja baada ya Chuo hicho  kutwaa ubingwa kwenye mashindano ya  (Shimivuta ) ambayo yalianza rasmi mnamo tarehe 10 disemba huko mkoani Iringa.

Nikwambie tu mnamo tarehe 8 disemba mwaka 2021 wanamichezo kutoka chuo cha (NIT)wakiongozwa na mwalimu wa  michezo Game tutor pamoja na wachezaji 45 waliondoka kuelekea Iringa kwa ajili ya kushiri mashindano hayo.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kilishiriki kwenye mashindano ya michezo ya aina tatu ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu na mpira wa pete.

Mwananchi scoop imezungumza na waziri wa habari kutoka chuo cha NIT Fanuel Kalinga na amethibitisha kutwaa ubingwa huo na kuzungumza haya kwa niaba ya washindi.

“Timu ya mpira wa wavu (Volleyball) walifanikiwa kuchukua kikombe cha mshindi wa kwanza bila kupoteza mchezo wowote Mpira wa miguu (Football) pia walifanikiwa kuchukua kikombe cha mshindi wa kwanza bila kupoteza mchezo wowote na Timu yetu ya mpira wa wavu (Netball) kwa wanawake ilifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali.”alisma

Hata hivyo walifanikiwa kupata Tuzo za vyeti kwa wachezaji bora akiwemo Tariq Mohamed  na mfungaji bora upande wa football James.

Ebwana eeeh!!! Hivyo ndivyo chuo cha NIT kilivyong’aa kwenye mashindano ya Shimivuta  kama mdau wa magazine ya mwananchi scoop unaweza kujifunza jambo kupitia mashindayo hayo kongole kwenu wababe NIT.

Mwananchi scoop inawatakia wafuatiliaji wote wa magazine yetu happy Friday na maandalizi mema ya siku kuu ya Christmas holaaaaaaaaa!!!!!!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags