Nina masters ujue...!

Nina masters ujue...!

Naam hiyo ndiyo kauli ya vijana wengi waliomaliza Vyuo Vikuu kwa ngazi hiyo ya Degree/Masters.

Hivi sasa kuna vijana wengi wamemaliza Degree au Masters ambao wapo kwenye soko la ajira. 

Kundi la vijana hawa kwa wingi wao wanahangaika mitaani wakitafuta ajira bila mafanikio na hivyo kuishi katika maisha magumu kupindukia wasijue la kufanya. 

Huu ndiyo mfumo wetu wa elimu ulipotufikisha.  Tunazalisha kundi la wasomi wanaotegemea kuajiriwa na siyo kuibua vipaji vya ubunifu wa kujiletea maendeleo.

Lakini hata hivyo bado wasomi hawa wana mkengeuko mkubwa wa kihaiba unaowadanganya kwamba ujuzi na maarifa ni kuwa na vyeti. 

Wasomi hawa wanadhani kuwa na vyeti ndiyo kila kitu na kusahau kujikagua katika utendaji wao pamoja na mitazamo yao kitabia na kimienendo. 

Kuna kitu kinaitwa attitude kwa kiswahili naweza kuita mitazamo katika utendaji wetu na tabia kwa ujumla. Vijana wengi waliosoma ngazi ya vyuo na kupata vyeti wanalo tatizo la kuwa na mitazamo hasi kwa kuamini kwamba vyeti vyao ndiyo vinavyowapa thamani na kusahau kwamba Sifa ya vyeti siku hizi haitazamwi sana kama sifa kuu ya kupata ajira.

Waajiri wengi hususan katika sekta binafsi wanaangalia attitude na kile mwajiriwa atakacho deliver. Vyeti vinakuwa ni vya kuthibitisha tu kama umepata elimu mujaarabu inayohusu taaluma fulani wanayoitaka na ndiyo maana kuna baadhi ya nafasi zikitangazwa hawasemi wanataka mtu mwenye masters pekee bali hutoa fursa kwa waliosomea taaluma hiyo kuanzia ngazi ya cheti,  diploma na shahada lakini msisitizo mkubwa ukiwekwa kwenye uzoefu kazini. 

Yapo makampuni makubwa ambayo yana vitengo vya  developmental learning program ambavyo vipo chini ya mkurugenzi au meneja rasilimali watu. 

Vitengo hivi kazi yake ni kuwachakata wafanyakazi bila kujali viwango vya elimu zao ili kuwaandaa kushika nafasi za juu pale fursa zinapotokea. Hii ni katika kukwepa kuajiri upya mara kwa mara hususan pale kampuni au shirika linapokua na kupanuka na zinapotokea nafasi za ngazi za juu huchukua wale wenye uzoefu ndani ya kampuni ambao wamefinyangwa ndani ya kampuni husika na kuiva na pia ambao wana positive attitudes na wenye kujiona kama ni miongoni mwa wamiliki au wana hisa katika kampuni (ownership)  

Kwa utaratibu huo makampuni haya huajiri vijana waliomaliza vyuo kwa ngazi mbalimbali katika nafasi za chini kabisa na hapo wanaingizwa kwenye huo mpango wa developmental learning program huku wakichunguzwa tabia zao kiutendaji.

Naam, hapo sasa ndipo unaposhuhudia vituko.

Kwa uzoefu wangu kazini na pia kupitia makampuni tunayohusiana kibiashara nimekuwa nikiwasiliana kikazi na baadhi ya makampuni hayo na kugundua udhaifu mwingi kwa hawa wasomi wetu. 

Kwanza ni "negative attitude" waliyo nayo kwa wale wanaodhani wamewazidi kielimu. 

Pili ni kudhani kwamba mpango kazi waliopewa na kusaini (job descriptions) ni biblia au msahafu ambao unapaswa kufuatwa kama ulivyo. 

Tatu ni kudharau kupuuza kujiunga na mpango wa developmental learning kazini kwa kujiona wamesoma sana hawahitaji kujifunza zaidi na dharau inakuwa kubwa zaidi pale wanapogundua kwamba wale waalimu wanaofundisha wamewazidi elimu. 

Vijana hawa hawapo tayari ku 'take initiative', kwenda extra mile inapotokea changamoto yenye kufikirisha,

Pia hawapendi kujitolea kufanya kazi muda wa ziada bila kutarajia malipo ya over time na hata kujitolea muda wao wa ziada kwenda kufanya kazi vitengo vingine ili kuongeza uzoefu kazini. 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Shaban Kaluse

A Sales and Marketing in the hospitality Industry and also a freelance journalist, writing about love and relationships and educative articles which aims for youths, every Tuesday on Mwananchi Scoop.


Latest Post