Nikiza Jr: Usiache shule kisa kipaji

Nikiza Jr: Usiache shule kisa kipaji

“Usiache shule kisa kipaji kwani utajilaumu maisha yako yote elimu ni muhimu sana unaposoma unaweka akiba kama ipo ipo tu jua kuna siku elimu itakutoa kukupeleka mahali ambapo hujagemea kwani wanavyosema elimu ni muongozo hawajakosea”

Hayo ni maneno ya kijana Justine Nikiza  maarufu kama Nikiza Jr ambaye ni Mwanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ( NIT) anayechukua  course ya Computer Science akiwa mwaka wa pili chuoni hapo.

Licha ya course anayochukua Nikiza Jr ni kijana  anayefanya sanaa akiwa na  Vipaji  zaidi ya vitatu ikiwemo Actor, Presenter na Master of Ceremony yaani MC lakini hajaacha kujikita kwenye elimu pamoja na kuwa na vitu vya ziada.

Wewe ni nani? Leo hii uone elimu si lolote si chochote kwako? Aiseee jitafakari kijana mwenzangu hii haimaanishi kuwa ambao hawana elimu hawawezi kusimama hapana wanauwezo tena mkubwa tu lakini ukijiimarisha kwenye elimu pia utakua umefanya bonge moja la Target mtu wangu.

“Kuna wakati nilikua naona kabisa mbona nikiacha chuo natoboa bwana lakini nakumbuka kaka yangu aliniambia kuwa soma kwanza kwani kuna wakati madili yako naweza kugoma halafu ikatokea mishe ya kazi ukaambiwa wanahitaji cheti tu halafu wewe ndo ulipotezea elimu”

“Hapo kiukweli unaona kabisa unapokosa ajira kizembe ukiacha shule unanafasi moja tu yakutoboa lakini ukisoma pia utakua na option mbili ukikosa huku unaangukia upande wa pili shule inahusika asikudanganye mtu” anasema

Unavitu vitatu kwa wakati mmoja vipi unaviwekaje hivi?

Hivi vitu ukijaribu kuangalia ni mambo ambayo yanaendana kama presenter na Mc ni vitu ambavyo vinashabihiana na acting pia havinipi ugumu navimudu vyote kwa pamoja”

Basi sawaa Nikiza wewe unafanya movie za aina gani?

“Napenda kufanya movie za Action coz sijawahi kujaaliwa kuwa romantic hivyo movie za romantic sitoboi kivileee kama nitakavyofanya za action kwani unaweza kujiuliza mshikaji anaigiza au ndo yupo serious kwa jinsi ninavyouvaa uhusika”

Hivi umeshawahi kufanya movie yoyote?

“Yes nimeshawahi kufanya na zipo ikiwemo ile ya Idris Sultan series nilicheza kama jamaa mwenye mapepo na niliigiza ukorofi ukorofi kama kawaida yangu

Soko la movie hapa nyumbani unalionaje?

“Soko la movie Tanzania liko chini kwani watanzania wanataka movie zinazoendelea nikimaanisha Series ambazo wanaziona kwa wenzetu hivyo wanazipa kipaumbele za nje kuliko za nyumbani”

“Mfano mdogo juzi hapa idriss ametoa movie yake kwenye Netflex  Slay support amepata lakini sio kama wenzetu wanavyofanya unakuta yani hata mtaani inaozungumziwa tofauti na hapa nyumbani muamko upo unatia moyo sio kivilee”anasema na kuongeza

“Hata hivyo muitikio upo coz kuna vitu ambayo watu wanahitaji tukitengeneza vizuri mimi naamin mabadiliko yatotokea tena makubwa tu”anasema.

Je unafikiri shida ni nini? Hadi kushuka thamani soko la movie

Shida ipo kuanzia kwenye production, quality  halafu watu wanataka waone uhaisia wa tukio kwa mfano mtu anapiga ngumi unasikia buuh hata ngumi haijafika kwa mlengwa  au mtu anapigwa mtama kabla haujafika tayari kadondoka”.

“kiukweli mambo kama haya yanakera sana nakumbuka kuna movie moja nilitizama ya hapa hapa kwetu mtu kapigwa risasi anachagua akafie wapi anangalia kabisa nataka kuanguka akiona mawe anakwepa anatafuta sehemu ambayo iko level watu wamechoka kuona mambo ya hivyo”anasema na kuongeza

“Hivi vitu vinashusha sanaa kwa kiasi kikubwa yani mtu anascript anasoma kabisa ambapo katika hali ya kawaida huwezi kuzngumza hivyo bhna kwa nini usiflow tu kama kawaida“anasema.

Kibongobongo ni movie gani ya action unaikubali?

“Aisee Agent Bavo iko vizuri kwani wamejaribu kutupa ule uhalisia wa matukio”anasema.

Muigizaji anayefanya action unamkubali

“Namkubali Lukamba licha ya kuwa camera man lakini anafanya movie za action na kubali sana action zake anazozifanya bhna”

Malengo yako ni yapi?

“Malengo ni kupata nafsi ya kushiriki kwenye movie kubwa za action ili nionyeshe uwezo niliokuwa nao lakini baada ya hapo nitasimama mwenyewe mana unaweza kutegemea kupata nafasi na ukakosa lazima nionyeshe mfano ili wajue kwanini nahitaji nafasi”anasema.

“Hata hivyo nategemea Mungu akijaalia watu waone movie yangu iko Netflix pale itakua bonge moja la kit undo ninachotamani pia “

Ni movie gani ambayo uliikosa kufanya na ikakuumiza

“Daah acha tu ni ile ya Awilo longomba inayokwenda kwa jina la Life to regret kwasababu muda ambao alikuja kushoot hapa bongo nilikua field sikuweza kuacha field kwa ajili ya kuja kufanya movie”

Changamoto unazozipata kwenye kazi yako

“Aisee acha changamoto ni kubwa sana kwani movie inahitaji muda sasa kutokana na mimi ni mwanafunzi wakati mwingine fursa zinatokea nashindwa kuacha masomo na kwenda kufanya”

“kuna muda unaambiwa unahitajika kambini wiki 2 inakua ngumu japo najitahidi mfano kama hizi za series inakua rahisi coz ni vipande nikipata nafanya naendelea na kitabu changu”anasema.

Lini ulianza kufanya maigizo?

“Hahahaha kitambo sana wakati nasoma Sekondary nakumbuka ili graduation ya form six nikiwa niko form 3 ndo nilianzia hapo tangu siku hiyo nilipongezwa na kupewa go ahead na wadau na walimu shuleni”.

Historia yake kwa ufupi

Nikiza Justine ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto watatu amemaliza elimu ya msingi katika shule ya  Nkololo “B” na kufanikiwa kujiunga Sekondary ST. Mary’s Nyegezi Seminary na Advance akasoma Hombolo Sekondary jijini Mwanza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post