Nigeria kama Marekani, Mabifu kila kona

Nigeria kama Marekani, Mabifu kila kona

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Kizz Daniel ameingia midomoni mwa watu baada ya majibizano yaliyotokea kati yake na msanii mwezie Tekno huku mashabiki wakidai kuwa Kizz alimtumia Tekno kuingiza maokoto kupitia wimbo wao wa ‘Buga’.

Minong’ono hiyo ilianza kupitia tweet iliyokuiwa ikisambaa katika mtandao wa X (zamani Twiter) imeeleza kuwa Tekno aliwahi kusema kuwa amekuwa akipatiwa asilimia 50 ya mapato kutoka wimbo wa ‘Buga’ hata baada ya mafanikio ya ziara yake alimtumia Naira bilioni 1 sawa Sh 1.8 bilioni huku akimlipa kila mwezi mapato yote anayoyapata kwenye Streaming Platforms.

Kutokana na tweet hiyo Tekno aliamka na kukanusha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa X akidai kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote huku akienda mbali zaidi na kudai kuwa Kizz Daniel hana fedha za kumlipa yeye.

Aidha Kizz naye hakulikalia kimya suala hilo aliamua kujibu akimtaka msanii huyo aache kumzungumzia kwani yeye ndiyo amemsaidia kurudi tena mjini kupitia wimbo wake wa ‘Buga’, hata hivyo Tekno alimjibu kwa kumwambia pia na yeye amuache kwa sababu ana siri zake nyingi atakuja kumdhalilisha.

Kizz Daniel na Tekno wamewahi kutoa ‘kolabo’ ya pamoja ya wimbo wa ‘Buga’ ambao ulitrend zaidi kupitia mitandao ya kijamii yenye zaidi ya watazamaji milioni 200 kupitia mtandao wa YouTube ikiwa na mwaka mmoja tuu tangu kuachiwa kwake.

Wiki hii nchini Nigeria kumeibuka mabifu kadhaa miongoni mwa wasanii kwa wasanii, ikumbukwe kuwa siku kadhaa zilizopita mwanamuziki Davido na Wizkid wamekuwa wakirushiana madongo kupitia mtandao wa X (zamani twiter) huku Davido akienda mbali zaidi akitaka yeye na Wizz watoe ngoma siku moja ili ijulikane nani mkali zaidi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags