Mwanamuziki kutoka Marekani, Nicki Minaj ameripotiwa kukabiliwa na kesi iliyofunguliwa na meneja wake wa zamani aitwaye Brandon Garrett ambaye amedai kuwa Minaj alimpiga wakati wa ziara yake ya 2024.
Kwa mujibu wa hati hiyo iliyowasilishwa katika mahakama iliyopo jijini New York imeeleza kuwa Nicki alimpiga kofi meneja wake huyo huku akimtamkia maneno ya kashfa yasemayo “Wewe ni mtu aliyekufa akitembea, Umeharibu maisha yako yote”.
Aidha msanii huyo hakuishia hapo licha ya walinzi kuingilia kati lakini alimshambulia kwa kuugonga mkono wake kwenye ukuta jambo ambalo lilimfanya meneja huyo kukaa chooni kwa lisaa limoja kwa aibu.
Garrett ameweka wazi kuwa lengo la kufungua kesi hiyo ni kutaka fidia kwani tukio hilo lilimuumiza kisaikolojia.
Utakumbuka kuwa 2024 Nicki alifanya ziara ya dunia aliyoipa jina la ‘Pink Friday 2 World Tour’ iliyoanza Machi mosi 2024 na kutamatika Oktoba 11, 2024.
Leave a Reply