Nicki Minaj hakamatiki kwenye mtandao wa spotify

Nicki Minaj hakamatiki kwenye mtandao wa spotify

Mwanadada Onika Tanya Maraj, maarufu Nicki Minaj amekuwa rapa wa kwanza wa kike kufikisha streams bilioni moja kwenye mtandao wa Spotify.

Minaj ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Trinidad iliyopo visiwa vya Carribean, amepata ‘streams’ nyingi kutoka kwenye albamu yake ya ‘Pink Friday 2’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka uliopita na kuchangia kufikia mafanikio hayo ya juu.

Nyimbo mbili kutoka kwenye rekodi hiyo, ‘FTCU’ na ‘Everybody’ aliyofanya na rapa Lil Uzi Vert bado zinaweka rekodi kwenye chati ya Billboard Hot 100 wiki hii.

Sehemu nyingine ya streams inakadiriwa kutoka kwenye wimbo wake wa pekee ‘Big Foot’ ambao ndio muziki mpya pekee alioutoa ndani ya mwaka 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags