Nicki Minaj agomea chanjo ya Corona

Nicki Minaj agomea chanjo ya Corona

Rapa kutoka nchini Marekani  Nicki Minaji ameweka wazi kwamba alikuwa na maambukizi ya virusi vya Corona hivi karibuni na kupelekea kutohudhuria kwenye Hafla ya ugawaji Tuzo za VMAS ambapo alitakiwa kutumbuiza.

Pia Nicki Minaj  amegoma kuhudhuria katika maonesho ya Mavazi, urembo(MET GALA 2021) huko New York akisema kuwa hawezi kujichanganya na watu wala kupata Chanjo ya  Covid 19.

Hata hivyo Rapa huyu amethibitisho hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kwamba atapata Chanjo hiyo mpaka pale atakaporidhishwa na Uchunguzi atakaoufanya, huku akiwashauri watu waendelee kujikinga kwa kuvaa Mask na kutojichanganya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags