Ni sawa matamasha ya muziki za injili kuwa na kiingilio

Ni sawa matamasha ya muziki za injili kuwa na kiingilio

Kumekuwa na baadhi ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikionesha baadhi ya watu kutofurahia malipo ya kiingilio yanayotolewa kwenye matamasha ya muziki wa injili. Kutokana na hilo mwimbaji wa muziki huo Walter Chilambo amesema hakuna ubaya wowote kwani inakuwa kama sadaka .

“Matamasha ya injili kuwa na kiingilio ni vizuri ni kama sadaka kanisani, tusipokuwa tunathamini vitu vya Mungu, alafu watu wanalipa viingilio baa na klabu inakuwa siyo vizuri na sisi inabidi tuwekeze.” Amesema Walter

Makali huu wa nyimbo za injili ambaye anafanya vizuri na vibao vyake kama vile Only you, Shwari, Sijawahi ona na vingine amesema kumtolea Mungu kwa njia ya sadaka ni kitu cha kawaida sana .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags